Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam inatarajia kutoa
uamuzi wa kupokea ama kutopokea kielelezo cha hati ya ukamataji nyumbani
kwa Wema Sepetu ifikapo Oktoba 4, 2017.
Hatua hiyo inatokana na kuwasilishwa kwa pingamizi mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba kutoka kwa wakili wa utetezi , Peter Kibatala,
kwamba kielelezo hicho kina mapungufu ya kisheria, hivyo kisipokelewe.
Kutokana na maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 4, 2017 kwa ajili ya kutoa uamuzi.
Wema Sepetu anashtakiwa kwa kosa la kukutwa na msokoto wa bangi pamoja na karatasi maalum za kuvutia dawa hiyo baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake.
Source http://www.bongomovies.com/kesi-ya-wema-sepetu-bado-ngumu/
![]() |
| Msanii Wema Sepetu |