-->

Alichokiandika Mc PiliPili kuhusu mtoto wa Marehemu Seth(Bikira Wa Kisukuma)

Alichokiandika Mc PiliPili kuhusu mtoto wa Marehemu Seth(Bikira Wa Kisukuma)



Baada ya majonzi mazito ya kifo cha aliekua mtangazaji wa kituo cha redio Efm marehemu SETH maarufu kwa jina la Bikira wa kisukuma Mc pilipili ameandika haya kupitia ukurasa wake wa picha instagram
"inaumiza...... mtoto wa Seth Mildred Giulians (Bikira wa kisukuma) huyu hapa"

akiwa msibani amemshika mtoto wa Bikila wa kisukuma wakiimba pambio zinazoimbwa malanyingi kwenye misiba pambio ya unapozulu wengine usinipite huku mtoto huyo akichezea ndevu za Mc pilipili.

"Basi Bikira wa Kisukuma alinambiaga niwe navunga hizi ndevu akaniambia hupenda kuzichezea kila akiwa nae basi mwanangu huyu hapa alipo anza kuzishika nami nikasafiri nikaenda mbali sana ila huyu mtoto tutasimamia mpaka akue asome ampendeze mungu na wanadamu ... seth in another fom"

mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi roho ya  marehemu Seth( Bikira wa kisukuma)
 
Back To Top