-->

Alichokisema Shamtha Kuhusu Diamond Kuzaa na Mobeto

Alichokisema Shamtha Kuhusu Diamond Kuzaa na Mobeto

Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ametia neno kile kinachoendelea kwa sasa kati ya Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.
Hamisa Mobeto

Mapema leo hii Diamond amekiri kuwa mtoto wa Hamissa ni mwanaye licha ya kuwa katika mahusiano na Baby Mama wake, Zari The boss Lady. Katika mtandao wa Instagram Shamsa ameandika ujumbe mfupi na kueleza kuwa Zari anastahili pongezi kwa kujua yote na kuamua kukaa kimya.
 "Kiukweli anasitahili pongezi kubwa sana, najaribu kuvaa viatu vyake kama mwanamke nayaona maumivu yake la pamoja na yote hakuna mwanaume asiyecheat. Zari endelea kumpenda Nassibu wako kamwe usimuache kwa ajili ya mwanamke mwenzio".
Ford ambae pia ni mke halali wa Chid Mpenzi aliongeza kwa kusema "Nchi yako ikivamiwa unatakiwa kupambana na si kukimbia"
mwanadada shamtha ford
Ujumbe wa Shamsa umekuja baada  post ya Steve Nyerere ambaye naye aliandika, “Wewe ni Malkia wa nguvu na yote yaliyopita bado umesimama na mmeo kuangalia watoto, Be Strong”.
 
Back To Top