-->

Gabo Zigamba ni kirusi kwenye tasnia ya filamu – Duma wa Siri ya Mtungi

Gabo Zigamba ni kirusi kwenye tasnia ya filamu – Duma wa Siri ya Mtungi


Msanii wa filamu aliyewahi kufanya vizuri katika Tamthilia ya Siri ya Mtungi  Michael  Duma amesema Gabo Zigamba ambae ni muigizaji bora wa filamu 2016 kupitia tuzo za EATV Awards, ni kirusi katika tasnia ya filamu.Duma amesema muigizaji huyo hawezi kuvaa vizuri na kujiweka kistaa hali  inayochafua tasnia ya filamu Tanzania
“Gabo ni kirusi popote alipo anajijua yeye ni kirusi lazima ajirekebishe na abadilike ukiangalia hajafanya kitu chochote kweny tasnia tangu amepewa tuzo, hata kwenye matukio makubwa hawezi kutokea kwasababu hata akialikwa haonekani kama ni staa,mtu kama yule anaweza kurudia suti mara tatu kwenye event kweli?”
Aliongeza,” kama anataka kubadilika abadilike kwasababu huwezi kuwa staa halafu unaishi maisha sawa na watu wa kawaida,”
Muigizaji huyo amedai yeye ni ‘anti Virus’ hivyo atajitahidi kurekebisha hali hiyo na kuwa mfano kwa wasanii wa filamu.

Bongo5
 
Back To Top