Bongo Movie inazidi kuwaka moto safari hii tena
hali inazidi kuwa ya balaa juu ya uwepo wa bifu wa Mwigizaji aliyetamba
na tamthiliya ya Siri ya Mtungi, Daudi Michael “Duma” pamoja na Gabo
Zigamba.
Duma amesema, Katika watu wa kwanza wanaoongoza
kuharibu sanaa ya Bongo Movie ni Gabo na sababu anayosema ni kuwa
hajitambui.
“Huyu jamaa ni kirusi katika tasnia yetu, angalia kwa mfano amepata
tuzo karibia nne,lakini ukiangalia haeleweki mpaka sasa amefanya nini
yaani hata ukimuona anapita huwezi kudhani kama ni staa wa filamu sababu
hajui kuvaa,” alisema.
“Gabo hana chakuongea, hata watu wanamuogopa kumuita katika sherehe
mbalimbali. Mtu gani anaweza kurudia suti zaidi ya mara tatu yani yupo
yupo tu anauza sura yaani haeleweki, kifupi kawaangusha Watanzania,”
aliongeza zaidi.
Upande wa Gabo akijibu tuhuma hizo anasema kwake hayupo tayari kumuongelea Duma kwa sababu yeye kaamua kumjadili.
“Sinaga urafiki kwanza na mwana taaluma ambaye tunafanana naye, ila
upo ujamaa tu lakini kwangu maneno hayana nafasi sana zaidi ya kazi.
“Akili ukiitumia vizuri unaweza kufanya mambo mengi ya maana, hivyo
si muda tutaona kipi ni kipi sababu mimi sijali sana maneno anayoongea
yeye, mimi nipo kikazi,” alisisitiza.


