WASANII kutoka kiwanda cha Filamu Tanzania wamejipanga kufanya Filamu ya kiistoria Nchini Sweden
Nyota hawa kutoka Tanzania wakiongozwa na Cloud 112 wamesema filamu hiyo itakua filamu ya kihistoria kutokana na maaandalizi waliyofanya katika uaandaaji wa filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ''USINISAHAU''
Akizungumza na kipindi cha e news cha east africa Television cloud amesema kisa cha filamu hiyo kitaelezea matatizo wanayo yapata watu wanao kwenda nchi za ugenini kutafuta maisha
''usinisahau ni story inayochoma moyo yani itaonyesha jinsi watu wanavyopata shida wakiwa ugenini kutafuta maisha yani Mdogo mtu haongei kaka mtu mlemavu na visa havijirudii jirudii na kila kisa kilichopo kina maana kubwa kuwepo"

