MUANDAAJI Wa video za Bongo Fleva kutoka Kwetu studio Maarufu kwa jina la ''Msafiri'' amesema sababu kubwa ya kudolola kwa Filamu za kitanzania ni ubora wa picha
Travela ambae amekua akitumiwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutengeneza kazi zao hasa zinazofanywa nje ya Tanzania amesema miaka ya nyuma watu walikua wananunua deki na dvd player kwajiri ya kutazama filamu za kitanzania tofauti na ilivyosasa
" Bongo movie imestack soko limeshuka mwanzo watu waliku wakinunua deki na dvd kwajiri ya kutazama bongo movie lakini sikuizi hazitumiki tena kutokana na ubora kuwa hafifu ukiringanisha na Bongo Fleva, labda tufanye vitu vipya na vizuri ndio tutawashawishi watanzania watazame na wazipende tena.
Msafiri ameongeza kuwa mziki wa tanzania hauwezi kudolola kama ilivo bongo movie kutokana na kila siku waandaji wanaongeza vitu vipya na vizuri zaidi.


