-->

OKOA FILAMU TANZANIA!

OKOA FILAMU TANZANIA!



Katika Comedy ambazo zimewahi kuzalishwa duniania Comedy ya HOME ALONE ndio Comedy pekee ambayo imeingiza mapato makubwa kuriko comedy zote duniani na bado hakuna comedy nyingine iliyowahi kutoka ikaizidi mapato! Watu wa Comedy mpo hapo?
Muvi ya TITANIC ilikuwa ndio muvi ya kwanza kuingiza pesa dola za kimarekani Bilion moja ikifuatiwa na AVATAR! Hapo ndipo huwa namvulia kofia James Cameron hana papara anapotaka kuzalisha filamu! Hana haraka

kabisa!
Tunajambo kubwa la kujifunza kwa kweli! Tunatumia muda mfupi kuzalisha muvi zetu na tunatumia muda mfupi zaidi kuingia location kuzalisha muvi nyingine! Ni lini Uingereza, Marekani, Japan, China, India, na kwingineko watakaa na kununua filamu zetu na kuzitazama na kufurahia? Tunadeni kubwa sana!!!
BODI ya Filamu Tafuteni watu wataalamu wa muvi ambao watakuwa makini kukagua kila muvi inayotakiwa kutoka bila kuwa na mazingira ya rushwa ili kuinusuru tasnia! Ili kama mtu atatengeneza muvi mbovu ina pigwa ban moja kwa moja isitoke ili wakurupukaji nao wafikilie sana kutengeneza kazi kwa umakini! Hiyo tabia yenu ya kukagua muvi dakika tu bila kutazama ubora wa muvi sio nzuri! Tokea muanze kukagua muvi ni muvi gani mliifungia? Ziko ngapi? Inamaana hizi zinazotoka ndio bora? Mbona watazamaji wana ng'amua makosa mapema na wanachukia? Ni viwango gani mlivyo weka kwenye hizo muvi? Bodi ni moja ya taasisi iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudolola kwa muvi zetu maana muvi zote mbovu na nzuri zimepitia kwao na wao waliona zinafaa kutazamwa na watu! Wakikagua muvi kwa ukali na zisizo faa wakazipiga chini naimani displine ya kuzalisha kilicho bora zaidi itakuwepo na tutakuwa serious tuache blah blah, 4,000/- ya mwananchi kwa sasa ni kubwa tu heshimu wanachotupa!

Homvye Junior Homvye

 
Back To Top